Habari za Punde

*DK. DIDAS MASABURI AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM

Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi (kushoto) akipongezwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya CXC Africa Limited, Charles Hamkah, wakati alipokuwa akipongezwa na ndugu, jamaa na marafiki baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Meya wa jiji uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo na kuwashinda wapinzani wake, Amir Mbunju, aliyejitoa na Grace Shelukindo. Masaburi ameibuka kidedea baada ya kuwamwaga wapinzani wake katika uchaguzi huo ambapo mpinzani wa kwanza ambaye ni Diwani wa Kata ya Tandale kupitia tiketi ya CUF, Jumanne Amri Mbunju, alijitoa katika kinyang'anyiro hicho na wapili, Grace Shelukindo Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala, alienguliwa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kuzingatia Kanuni na Sheria ya Serikali ya Mitaa namba 8 iliyoundwa mwaka 1982, isemayo Meya wa Jiji ni yule anayechaguliwa kutoka katika Kata na Haimpi fulsa ya kushinda anayetoka Viti Maalum. Jumla ya wajumbe walikuwa ni 129, waliopiga kura walikuwa ni 125 na wanne kati yao hawakupiga kura na Kura zilizoharibika ni 9 za Hapana ni 13 na za Ndiyo ni 103.
Dk Didas Masaburi, akipongezwa na mkewe, Janeth Masaburi baada ya ushindi huo.
Dk. Didas, akivishwa taji na mtoto wake, Christina Masaburi, baada ya ushindi huo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.