Rapa mahiri aliyeibukia beni ya Extra Bongo na kutamba na bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' baada ya kuyumba kwa bendi ya Etxra, Khalid Chokoraa, ambaye kwa siku za hivi karibuni alitangazwa kuwa amesimamishwa na uongozi wa bendi yake ya Twanga kwa kile kilichodaiwa utovu wa nidhamu na kuwa akifanya maonyesho na bendi yake binafsi iliyoibuka hivi karibuni ya Mapacha Watatu, sasa ametimuliwa rasmi katika kikosi hicho cha Twanga baada ya kusimamishwa na kudaiwa kujiunga na bendi yake ya zamani ya Extra Bongo, iliyochini ya uongozi wa Ally Choki. Mbali na Chokoraa pia mwingine aliyeondolewa katika kikosi hicho kwa tuhuma kama hizo ni Kalala Junior ambaye naye amedaiwa kujiunga na Extra Bongo.
TAIFA STARS YATOA SARE 1-1 NA UGANDA AFCON
-
TANZANIA na Uganda zimegawana pointi kwa sare ya kufungana bao 1-1 katika
mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) usiku huu
Uwanj...
6 hours ago
No comments:
Post a Comment