Uongozi na WAfanyakazi wa Paradise All Suites Hotel, kwa kushirikiana na Angella Bondo Show (kipindi kilichopewa msukumo na kipindi cha Oprah Winfrey) wanawakaribisha katika “Christmas Lunch” , mlo utakaojumuisha kuanzia Break Fast asubuhi na mlo wa mchana, itakayofanyika Jumamosi ya tarehe 18, Desema 2010.Meneja wa hoteli hiyo, Anold Lema, amesema kuwa siku hiyo itakuwa mahsusi kwa wapendanao na kuwafurahisha tuwapendao hivyo ni siku itakayokuwa na mambo mbalimbali ikiwamo michezo ya kina mama, watoto na marafiki wote watakaojumuika na binti zao. Michezo hii itawasaidia kina mama hawa kutumia muda huo kukaa na kufurahi na wale wawapendao katika msimu huu wa sikukuu.
Tiketi za kiingilio tayari zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini, Hoteli hii ya Paradise ipo Paradise katika jengo la Benjamin Mkapa katikati ya jiji na Chicken Hut Mlimani City. Wote mnakaribishwa kujumuika katika Sherehe hii.
Ticketi ni Sh 30,000 kwa mtu mmoja
No comments:
Post a Comment