
Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakichagua nguo katika mtaa wa Kongo leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sikukuu ya Krismas. Wakazi wengi wa jijini wamekuwa wakinunua nguo za mitumba zaidi kutokana na kupanda bei kwa nguo za dukani na hasa nyakati za Sikukuu.

Gari dogo likiwa limesheheni mizigo na miti ya Krismasi likiingia maeneo ya katikati ya jiji Kisutu Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuanza kuuza miti hiyo inayotumika kwa mapambo wakati wa Sikukuu ya Krismasi inayosherehekewa Desemba 25 kila mwaka duniani kote. Hata hivyo soko la miti hiyo siku hizi limepungua kutokana na kuwapo kwa miti mingi ya Atifisho ya Kichina.

Wakazi wa jijini Kinamama, wakiwa na watoto wao wakichagua viatu Mtaa wa Kongo.
No comments:
Post a Comment