Kundi hilo limewasili nchini kwa ajili ya maonyesho matatu na bendi ya Rufita Connection iliyo chini ya uongozi wa Banza Stone kuanzia kesho kabla ya kuelekea mikoani. Kundi hilo linatarajia kuanza kufanya onyesho lake la kwanza katika Ukumbi wa Land Mark Ubungo siku ya Ijumaa Desemba 17, na onyesho la pili litafanyika Desemba 18, kwenye Ukumbi wa Rufita Night Club Rufita, Tabata Segerea na latatu litafanyika kwenye Ukumbi wa Rainbow Club uliopo Mbezi Beach Desemba 19, na Desemba 21 watafanya onyesho lao Ifakara na desemba 22 watashambulia Morogoro mjini.
Akizungumza na Sufianimafoto Meneja Masoko wa Kampuni ya Rufita Entertinment & Promotion, Juma Abajalo, alisema kuwa bendi hiyo itapiga live na bendi ya Rufita inayoongozwa na Banza Stone katika maonyesho yote, ambapo baada ya kukamilika kwa maonyesho hayo matatu ya jijini, bendi hiyo itaelekea mikoani baada ya kumaliza ratiba yake ya Sikukuu ya Krismas. Mkesha wa Sikukuu Makhirikhiri watashambulia katika ukumbi wa Msasani Club.
No comments:
Post a Comment