Habari za Punde

*WANAFUNZI WA IFM NA ISLAMIC MOROGORO WAVAMIA OFISI ZA BODI YA MIKOPO

Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Machunda Lubambula. akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha IFM, wakati akitoa majibu kuhusu malalamiko yao, wakati walipofika kwenye ofisi hizo Msasani jijini Dar es Salaam leo mchana.
Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo vikuu vya IFM na Chuo cha Waislam Morogoro, wakihamaki wakati walipokuwa nje ya Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilizopo Msasani jijiji Dar es Salaam leo mchana, walipofika kuulalamikia uongozi wa bodi hiyo kwa kutosimamia taratibu za ulipaji wa ada za wanafunzi na kupanda kiholela kwa ada kutoka Sh. milioni 1 hadi milioni 1.7, jambo linalowafanya baadhi ya wananfunzi kushindwa kulipa.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.