
Baadhi ya Maafisa Habari Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa pembeni ya Mto Kiwira jana wilayani Rungwe kwa ajili ya kujionea maajabu ya Daraja la Mungu ambao maji ya mto huo yanapita katikati yake. Maafisa hao walifanya ziara ya mafunzo kwa lengo la kujifunza na kujionea vivutio.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO 
Mmoja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Pili Rajab akielezea kufurahishwa kwake na maajabu ya Ziwa Ngosi baada ya kujionea (nyuma yake) lilipo katikati ya milima na kulifanya lifanane na Ngorongoro Crater. Mfanyakazi huyo na Maafisa Habari wa Serikali walikwenda Wilayani Rungwe jana kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya vivutio mbalimbali vilivyopo wilayani humo.

Baadhi ya Maafisa Habari Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufikia kilele cha Mlima Uporoto ambao unazunguka Ziwa Ngosi. Ziara hiyo ya mafunzo ilifanyika jana kwa lengo la kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vya wilayani humo kwa ajili ya kuvitangaza ili visaidie kuongeza pato la Taifa.
No comments:
Post a Comment