Habari za Punde

*MATUKIO YA JIJINI DAR LEO

TIGO NA HELA YA FASTAFASTA YA SIKUKUU Askari wa doria (Tigo) akimuhoji mwendesha pikipiki aliyekuwa akipita pembeni mwa magari yaliyokuwa yamesimama Barabara ya Mandela kwenye taa za makutano ya Barabara hiyo na Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Haikuweza kufahamika kosa la dereva huyo.
UKUTA ULIOPEMBENI YA HOSPITALI YA AGHAKHAN WAVUNJWA
Mafundi wakiondoa matofali baada ya kubomolewa ukuta uliokuwa umejengwa pembezoni mwa Hospitali ya Agakhan Dar es Salaam. Ukuta huo na ule uliokuwa umejengwa mbele ya Hoteli ya Palm Beach, ulibomolewa jana kwa agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Anna Tibaijuka.

MADEREVA WASIOFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
Dereva wa daladala linalofanya safari zake Mwenge Posta, akitanua pembeni ya barabara eneo la Makumbusho, baada ya kukuta foleni kubwa eneo hilo bila kujali usalama wa waenda kwa miguu.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.