Habari za Punde

*TID NA TOP BAND KUZINDUA ALBAM YAO YA SIFAI DESEMBA 28

TID SHOW BIZMSANII wa miondoko ya Bongo Flava Khalid Mohamed, maarufu kama TID, na bendi yake ya Top Band, anatarajia kuzindua albam yake inayokwenda kwa jina la Sifai itakayokuwa na jumla ya nyimbo nane.
Akizungumza na Sufianimafoto TID, alisema kuwa uzinduzi wa albam hiyo unatarajia kufanyika Desemba 28 Mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Club Billicanas.
Aidha alisema kuwa katika uzinduzi huo atasindikizwa na wasanii wa miondoko hiyo aliowataja kuwa ni pamoja na Lady Jay Dee na bendi yake ya Machozi, Sam wa Ukweli, Albert Mangwair, Jay Moe pamoja na wasanii wengine kibao.
Alitaja kiingilio cha kuwezesha kuonya Shoo hiyo kuwa ni Sh. 7000 kwa mtu mmoja, ambapo shoo hiyo itaanza saa tatu usiku hadi majogoo.

Baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo la bendi ya 'Top Band' wakipozi kwa picha.

Kava la CD ya almba hiyo itakavyokuwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.