Habari za Punde

*MSHIRIKI WA TUSKER PROJECT FAME PETER MSECHU AWASILI DAR

Mshiriki wa mashindano ya Tusker Project Fame, Peter Msechu, akifurahia baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo mchana akitokea nchini Kenya. Msechu aliyeshika nafasi ya pili katika mashindano ya Tusker Project Fame yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Kenya,
Katika mashindano hayo, Msechu alishika nafasi ya pili nyuma ya Levis Ntare wa Uganda, aliyekamata nafasi ya kwanza.
Msechu, akifurahia baada ya kutoka nje ya Uwanja huo na kukuta nyomi la wabongo, Ndugu jamaa na marafiki wakisubiri kumlaki.
Hata mshikaji wake Jackson George, aliyekuwa naye katika kinyang;anyiro cha kumska mkali wa Bongo Star Search, pia alikuwapo uwanjani hapo katika kuhakikisha anakamilisha furaha ya mchizi wake Msechu pindi atakapo wasili, na hapa Jackson (kushoto) akipozi kwa picha na Kaka wa Msechu (kushoto).
Msechu akipunga mikono kwa furaha kuwasalimia mashabiki wake na wananchi waliojitokeza kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo, ambapo baada ya hapo msafara wake ulipita katika baadhi ya mitaa kuelekea Redio Clouds kwa mahojiano.










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.