Habari za Punde

*NOKIA, VODACOM WAUNGANA KURAHISISHA MATUMIZI YA INTERNET KATIKA SIMU ZA NOKIA C3

KAMPUNI ya simu za Nokia kwa kushirikiana na Kampuni ya mtandao wa simu wa Vodacom Tanzania, wamezindua huduma mpya itakayomuwezesha mteja kutuma ujumbe mfupi kupitia intaneti, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kuchati.
Uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, ulihusisha pia uzinduzi wa aina mpya ya simu za Nokia ya C3 yenye kasi kubwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja mawasiliano wa Nokia kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kusini, Doroth Ooko, alisema Nokia wameamua kushirikiana na Vodacom ili kuwafikia watu wengi zaidi na kuhakikisha kuwa watanzania wanaungwanisha na sehemu nyingine ya Dunia.
“Simu hizi za C3 ni moja kati ya ubunifu wa juu kuwahi kutokea,pamoja na spidi kubwa iliyokuwa nayo, aina hii ya simu ni imara na itakayomuwezesha mtanzania kuwasiliana na mtu yeyote mahala popote duniani.
“Kwa sasa tunafanya juhudi kubwa kuishawishi Serikali ipunguze kodi thamani (VAT) katika simu hizi. Lengo letu hapa ni moja tu, kuwawezesha watanzania wote waweze kumudu, licha ya vipato kutofautiana,”alisema Ooko.
Nae Meneja Mawasiliano wa Vodacom, Nector Foya, alisema, wameamua kushirikiana na Nokia kwa kuwa wanatambua mahitaji ya wateja wa mtandao wao.
“Tunajua nini wateja wetu wanahitaji, na kama ambavyo imekuwa kawaida yetu, tunafanya juhudi kuhakikisha wateja wa Vodacom, wanaendelea kupata bidha bora zaidi.
“Huduma hii mpya, itampa mteja wa wetu fursa ya kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki kwa namna ya aina yake, kwani pamoj na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, sasa atapata nafasi ya kutumia intaneti bure, na kuchati kwa mara moja,”alisema Foya.
Alisema kwa sasa Vodacom ina mpango kabambe wa kuhakikisha kuwa wateja wake wanakuwa wakwanza kupata kila huduma bora itakayoanzishwa.

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Nector Foya (kushoto) akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo iliyoungana na mtandao wa vodacom wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Nje Vodacom, Upendo Richard, akisoma hotuba yake kuhusu huduma hiyo.
Meneja Mauzo wa Nokia Tanzania, Kishor Kumar, akimkabidhi mshindi wa Droo iliyocheeshwa maalum kwa ajili ya waandishi wa habari waliohudhulia hafla hiyo na kujinyakulia simu mpya ya C3.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.