Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akisalimiana na bwana harusi Abdul Mohamed, aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Dimba linalochapishwa na Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, wakati wa sherehe ya harusi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo mchana. Abdul alifunga ndoa na mkewe Mulhat Seif jana usiku,
Bi Harusi Mulhat Seif akiwa na msimamizi wake, Lutfiya Hamid, wakati wa sherehe hiyo leo mchana.
"Karibu kwenye Ulimwengu maridhawa wa Maisha Bora kwa kila mwenye ndoa"!
"Ebwana eeeh! hongera sana kwa kuwahi kutangaza nia kabla yangu na kuwin, mie mwenzio mwezi wa tano mwakani nitakuwa kama wewe" teh teh teh!
Mwandishi mwandamizi na mhariri wa gazeti la Champion, Saleh Ally 'Muneke', akimpongeza Abdula Mohamed kwa kumuwahi kuchukua jiko.
"Aaah! Mhariri wangu hongera sana, umetuonyesha mfano bora nasie tutafuata, ila mie mwenzio bado nipo nipo saaana tu kwani wala sijui kati ya wale wakinananiliu nimchague nani"
Mhariri msaidizi wa Champion, Elius Kambili, akimpa Big Up, aliyewahi kuwa mhariri wake wakati akifanya kazi Kampuni ya New Habari kabla ya kuhamia Global Publishers.
"Wala usijali mshikaji wangu na mie nipo nyuma yako, ila yangu nadhani itakuwa ni mwezi wa nane mwakani, si unajua mambo yalivyokuwa magumu? najipanga kwanza"
Vicent, akimpongeza Abdula, kwani watu hawa walihsawahi kufanya kazi pamoja kampuni ya New Habari.
"Kaka Hongera sana, ila mie usiniulize ntaoa lini ntakuwa sina majibu ya fasta fasta, usijientia aibu bure"

No comments:
Post a Comment