Habari za Punde

*TASWA FC YAKABIDHIWA JEZI ZA KUSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI

Mratibu wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi, yanayotarajia kufanyika mjini Zanzibar, Othman Kazi, (kushoto) Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya Azania, Mohammed Bashrahil (wapili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni hiyo, Awadh Fuad (wapili kulia) wakimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo (jezi) Mwenyekiti wa timu ya Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania Taswa Fc, Majuto Omar, kwa ajili ya timu hiyo inayokwenda kucheza mchezo wa kirafiki na Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi Januari 12. Vifaa hivyi vinathamani ya Sh. milioni 2.6, na hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika kwenye Mgahawa na Hadees Dar es Salaam leo mchana.
Othman Kazi, akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo la kukabidhi vifaa hivyo.

Na Mwandishi Wetu, Jijini
KAMPUNI ya Ngano Azania imekabidhi jezi seti nne kwa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC), Baraza la Wawakilishi, Tanzania Stars na timu ya Zanzibar Veterani kwa madhumuni ya kutumika katika mechi maalum za kusheherekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jezi hizo zilikabidhiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Ngano ya Azania, Mohamed Bashrahil katika mkutano na waandishi wa habari jana uliofanyika kwenye ukumbi wa Hadees.
Bashrahil alisema kuwa sababu kubwa ya kutoa msaada huo ni kutambua umuhimu wa maendeleo ya michezo nchini na vile vile kama sehemu yao ya kutambua Muungano wa Tanzania na hasa Sikukuu ya Mapinduzi.
Alisema kuwa sikukuu ya Mapinduzi ni kielelezo ya Muungano thabiti wa Tanzania Bara na Visiwani na wao kama kampuni ya Muungano inayofanya kazi zake katika sehemu zote mbili.
“Masoko yetu yapo Tanzania Bara na Visiwani, tunaamini kwa kupitia msaada huu, watanzania watatambua nini tunafanya japo tupo katika biashara muda mrefu sasa, msaa
da huu ni kielelezo tosha cha kutambua Muungano thabiti,” alisema Bashrahil.
Alisema kuwa jezi seti nne zina thamani ya sh. Milion 2.4 na mbali ya hizo jezi, watasaidia vifaa mbali mbali kama kofia, fulana na jezi za kupashia viungo moto au warm up.’
Kwa mujibu wa Bashrahil, wataendelea kusaidia michezo kwani msaada huu ni mwanzo tu wa kielelezo cha ubora wa bidhaa zao na kampuni kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada mkubwa waliotoa kwani wanaamini timu zote nne zitapendeza siku ya sikukuu hiyo.
Majuto alisema kuwa “Sikukuu bora ni kuvaa nguo mpya” hivyo wanaamini kuwa msaada huo utaongeza ari za wachezaji na kuibuka na ushindi siku hiyo.
Mkurugenzi wa Popular Sports and Entertainment Tanzania (PSET), Othman Kazi aliishukuru kampuni ya Azania kwa msaada huo na kwani imechangia kufanikisha adhma ya kampuni yake iliyoandaa mechi hizo maalum.
Kazi alisema kuwa ni heshima kubwa kwa kampuni ya Azania na kupunguza ‘presha’ ya bajeti kubwa ya PSET iliyoandaa shughuli hiyo.
“Naziomba kampuni nyingine ziunge mkono Azania na kusapoti PSET ili kufanikisha shughuli hiyo nzito na muhimu kwa Watanzania,” alisema Kazi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.