Habari za Punde

*WACHINJAJI VINGUNGUTI WAGOMA KUCHINJA

Hawa ni baadhi tu ya Ng'ombe waliotakiwa kuchinjwa kwa siku ya leo wakiwa wamezagaa ndani ya uzio wa Machinjio hayo baada ya wachinjaji hao kugoma kuchinja ng’ombe leo, kwa kile walichodai matatizo ya mgawo wa umeme ambao huwaweka katika mazingira magumu ya kufanya kazi hiyo ya uchinjaji inayoanza saa nne usiku hadi asubuhi. Pia wachinjaji hao wameilalamikia Manispaa ya Ilala kutotengeneza jenereta lililoharibika kwa kuda mrefu sasa, ambalo lingeweza kuwasaidia kipindi hiki cha mgawo.
Hawa ni baadhi ya wafanyabiashara wakikokota wenyewe mbuzi wao kuingiza machinjioni ili wachinjiwe kwa ajili ya kupeleka katika biashara zao kwenye Mabaa na Sehemu za Starehe.
Wachinjaji wakiwa katika Machinjio ya Vingunguti, jijini Dar es Salaam, wakichinja mbuzi kwa ajili ya matumizi ya baa na sehemu za starehe.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.