Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha CUF (JWCUF), Nuru Bafadhil, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mchana, wakati wakitoa tamko kwa UWT na Taasisi za Wanawake nchini zinazotumia majina ya kinyume cha malengo yaliyokusudiwa. Waliutaka Umoja wa Wanawake, (UWT) kubadili jina hilo wakidai linawanufaisha zaidi wanawake wa CCM pekee na si walengwa wote.Kushoto ni Ofisa Uratibu na Makundi, Dahwa Majid.
Aidha alisema kuwa Taasisi zinalizojisajili kwa lengo la kusaidia Wanawake zifanye hivyo bila kujali itikadi za Vyama vya Siasa na dini.
"Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuandaa sherehe za Siku ya Wanawake Duniani, kwa kugharamia chakula, burudani pamoja na kunywa na kuwafurahisha baadhi tu ya wanawake hali ya kuwa walengwa wamesahaulika na wala hawahusishwi katika sherehe hizo ambao wengi wao ni wale walio vijijini ambao hawafaidi matunda yao ya UWT,
Kwa hiyo tunaiomba Serikali kusimamia na kuangalia usajiri na utendaji wa Baadhi ya Taasisi zinazotumia tu majina ya wanawake ili kujinufaisha binafsi bila kuwajali wanawake kama ambavyo zimejiandikisha" alisema Nuru.

No comments:
Post a Comment