Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari (TASWA) Maulid Kitenge, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, wakati akitoa utaratibu wa michezo itakayochezwa katika Bonanza la waandishi siku ya Jumamosi kwenye Ufukwe wa Coco Beach. Kulia ni Katibu wa Chama hicho, Amir Mhando.
*Wahariri kushindana kufukuza upepo
Na Sufianimafoto Reporter, jijini
WAZIRI wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza la vyombo vya habari litakalofanyika Dar es Salaam.
*Wahariri kushindana kufukuza upepo
Na Sufianimafoto Reporter, jijini
WAZIRI wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza la vyombo vya habari litakalofanyika Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando alisema Waziri Nchimbi atatoa zawadi kwa washindi mbalimbali kwenye bonanza hilo litakalofanyika eneo la Coco Beach kuanzia saa nne asubuhi hadi saa mbili usiku.
Mhando alisema pia katika kuboresha bonanza hilo, wameweka kipengere cha mashindano ya mbio za meta 100 kwa ajili ya wahariri na kwamba mshindi wa kwanza atapewa medali ya dhahabu, wa pili fedha na wa tatu shaba.
“Lakini wahariri ni wale ambao umri wao kidogo unaelekea katika miaka 50 ama zaidi, hivyo tumewasiliana na viongozi wa Jukwaa la Wahariri watusaidie katika hili.
“Wametuahidi watatupa sapoti kuhamasisha wahariri wajitokeze zaidi kushiriki kwenye bonanza na hasa kwa mbio za meta 100,” alisema Mhando.
Alieleza kuwa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ itatumbuiza kwenye bonanza hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na kuandaliwa na TASWA.
Alisema michezo mbalimbali itashindaniwa ambayo ni soka ya ufukweni (wanaume), netiboli (wanawake), wavu (jinsia zote watachanganyika), mbio za magunia (wanawake na wanaume), mbio meta 100, kuruka kichura (wanawake na wanaume) na kuvuta kamba (jinsia zote watachanganyika) na kucheza muziki (wanawake na wanaume).
Kwa mujibu wa Mhando michezo yote itakuwa na zawadi ya vikombe isipokuwa kucheza muziki zawadi yake ni fedha taslimu.
No comments:
Post a Comment