Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofosi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza leo. Pembeni ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Chabaka Kilumanga, mwenyeji wa Spika Ubalozini. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza na maafisa wa Ubalozi wetu Uingereza mara baada ya kuwatembelea
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga baada ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Pembeni ni mjumbe wa kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Beatrice Shelukindo aliyekuwa ameambatana na Mhe. Spika.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifurahia jinsi picha mbalimbali za Mabalozi wa Tanzania waliowahi kuhudumia Ubalozi wetu tangu Uhuru nchini Uingereza zilivyopambwa katika ngazi za kuingia Ubalozini hapo mara baada ya kutembelea Ubalozi huo Leo. Anaemuongoza kuingia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga pamoja na watumishi wote wa Ubalozi wetu nchini Uingereza mara baada ya kutembelea Ubalozi wetu Uingereza.
No comments:
Post a Comment