Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMJULIA HALI MALECELA MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu John Malecela, alipofika kumjulia hali nyumbani kwake mjini Dodoma jana. Mzee Malecela alifanyiwa upasuaji nchini India na hali yake inaendelea kuimarika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela, wakati alipofika nyumbani kwake mjini Dodoma jana, kmjulia hali baada kufanyiwa upasuaji nchini India hivi karibuni. KMshoto ni Mama Asha Bilal.
Mama Asha Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake mjini Dodoma na Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia).
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (kulia) akifurahia jambo na mke wa  Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela,Anne Kilango.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mke wa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela (wa pili kulia) ambaye pia anaagana na mke wa Kamau wa rais Mama Asha Bilal, baada ya mazungumzo wakati walipofika nyumbani mstaafu huyo mjini Dodoma jana, kumjulia hali baada kufanyiwa upasuaji nchini India hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.