Habari za Punde

*WANAFUNZI WA UDOM WASOTEA VITAMBULISHO VYA KUREJEA CHUONI

 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (U-Dom) wakiwa katika foleni ya kujiandikisha upya na kupatiwa vitambulisho vipya pamoja na namba za kurejea chuoni baada ya wanafunzi hao kuanza kurejea mjini  Dodoma. Wanafunzi hao waliandaliwa utaratibu wa kujiandikisha upya ikiwa ni pamoja na kuhakikiwa kuhusu malipo ya Ada, pamoja na kuapishwa na Wanasheeria wakiapa kuwa hawatarudia tena kugoma.
 Askari Polisi akiwaarati baadhi ya wanafunzi ili kukaa katika foleni na wasiweze kuchakachua na kurukia foleni za wenzao wakati wa mchakato huo, ulifanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 "Duh! Hata foleni yenyewe haisogei.....?" Baadhi ya Wanafuzi waliochelewa kuchukua namba ya kuingia kwenye usaili huo,wakichungulia kwenye moja ya mageti ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Hawa ndo kwanza wamejichokea kusubiri utaratibu wa kuitwa ili kuanza hatua ya mwanzo ya ukaguzi wa Ada.
Wengine waliochelewa kuchukua namba wakiwa nje ya geti kuu la kuingilia kusubiria taratibu ya viongozi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.