Habari za Punde

*ABBAS KANDORO AANZA KAZI KWA ODA MKOA WA MBEYA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoroakipokea nyaraka na mikoba tayari kwenda kuanza kazi katika mkoa mgumu wa Mbeya, wakati akiapishwa wiki iliyopita. 
Kandoro aliyewahi kuongoza mikoa migumu kama Jiji la Dar es Salaam na Mwanza, hivi sasa mara tu baada ya kuwasili mkoa huo wa Mbeya ambao pia ni miongoni mwa mikoa migumu na inayoongoza kwa matukio, ajana ametoa agizo kwa wananchi wote waliojenga kwa matofali kiholela katika eneo linalodaiwa kuwa lina kesi mahakamani ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakiendesha biashara katika eneo hilo. 
Aidha Kandoro amepokewa kwa baadhi ya matukio makubwa mkoani humo kama majanga ya moto ambayo yametokea hivi karibuni na kuteketeza vibanda vya biashara na baadhi ya wananchi kujeruhiwa katika matukio mbalimbali.
 Moto ukiteketeza baadhi ya vibanda vya biashara eneo la Forest mkoani Mbeya hivi karibuni.
Mmoja kati ya watu walioumizwa katika matukio ya vurugu kwa kupigwa na nondo, mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.