Helkopta ya kampeni za CCM ikitua katika Uwanja wa Sabasaba mjini Igunga leo, ambapo iliwasili ikiwa na Katibu wa NEC, Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge wa Bumbuli (CCM) Januari Makamba pamoja na John Pombe Magufuli.
Helkopta ya CUF ikiwa imetua katika Kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga, ilikuwa ni baada ya kuwasili mjini Igunga na kuanza kazi za kampeni mara moja.
Mratibu wa Kampeni za CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akimlaki Januari Makamba baada ya helkopta aliyokuja nayo kutua kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Igunga. Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.
Waziri wa Ujenzi ,John Magufuli, akisalimia mamia ya wananchi waliofika kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Igunga kupokea Helkopta ya kampeni za CCM.Wengine ni Nchemba na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma.
Januari Makamba akisalimia mamia ya wananchi waliofika katika mapokezi ya helkopta ya kampeni za CCM ilipowasili leo asubuhi kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini.
Mamia ya watu katika uwanja wa sabasaba mjini Igunga katika mapokezi ya helkopta ya CCM.
Hii ni moja ya sababu zilizofaya baadhi ya vyama vya siasa kujitahidi kwa kila hali kuweza kufika katika maeneo husika kwa kutumia usafiri wa anga kutokana na ubovu wa barabara. Waziri wa Ujenzi Hohn Magufuli tayari amekwishaahidi kujenga Daraja katika eneo hili la Mbutu.
No comments:
Post a Comment