Matukio ya ajali yanaendelea kuiandama mikoa ya Kusini hususan mkoa wa Mbeya, ambapo leo tena jumla ya watu zaidi ya nane kufariki papo hapo na wengine zaidi ya 23 kujeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya baada ya gari aina ya Costa waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na Prado usiku wa kuamkia leo.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu kutoka eneo hilo la ajali shuhuda wa ajali hiyo ambaye ni miongoni mwa abiria waliokuwamo katika gari hilo, anasema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili za usiku katika eneo la Ihanda Tunduma mkoani Mbeya na kuitaja Costa hiyo kuwa ni kampuni ya Mbombo .

Aidha shuhuda huyo alisema kuwa chanzo cha ajlai hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa Costa hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa spidi isiyokuwa na kikomo na Controral zaidi na kuwa akiovertake bila utaratibu kila mara.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Meya Advocete Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa taarifa zaidi itatolewa baada ya kufika eneo la tukio japo alisema majeruhi wa ajali hiyo na maiti zimehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Mbozi.
No comments:
Post a Comment