Mwenzagu Pokea pete hii iwe ishara ya upendo wangu kwako na uaminifu wangu kwako. Ndivyo inavyoonekana Rahma akitamka maneno hayo wakati alipokuwa akimvisha pete ya ndoa mumewe Ibra Kaude, baada ya kufungishwa ndoa Katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe Mkoani Morogoro.
Sherehe ya kuwapongeza ilifanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Jumapili ya septemba 11. Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania. Picha na Albart Jackson
Maharusi Ibra Kaude, akiwa na mkewe, Rahma Othuman Mohammed wakionyesha shahada za vyeti vya Ndoa baada ya kufunga ndoa yao katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe Mkoani Morogoro.
Ibra Kaude na mkewe Rahma Othumani Mohammed wakiwa katika pozi la picha wakati wa sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, maharusi hao walifunga ndoa yao siku ya ijumaa ya tarehe 9 katika msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe Mkoani Morogoro.
Ibra na Rahma, wakiingia ukumbini Kajimjee wakati wa sherehe ya kuwaongeza.
Ibra na Mkewe Rahma wakikata keki iliyoandaliwa kwa maalum kwa ajili yao wakati wa sherehe ya harusi yao iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kaka wa bibi harusi Rahma Othuman, Hifidh Othumani akimfungisha ndoa Ibra Kaude (kulia ) huku wakiongozwa na sheikh kutoka bakwata jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment