Habari za Punde

*MAFUNZO YA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO (TASWA) YAMALIZIKA MOROGORO

Mmoja wa waandishi wa habari wa michezo akijibu swali aliloulizwa na Mwalimu wa mafunzo hayo mkufunzi,  Said Salim (kulia) wakati wa semina ya kuwanoa waandishi wa habari za michezo  wanaoshiriki semina hiyo  iliyoandaliwa na Taswa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Mjini Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa  habari za michezo, Jenifer Ulembo (kulia) na Zaituni Kibwana, wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na Taswa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Mjini Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa  habari za michezo wakiwa katika semina ya kuwanoa waandishi wa habari za michezo  iliyoandaliwa na Taswa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Mjini Morogoro.
********************
MKUU wa Mkoa wa  Morogoro Joel Bendera amewataka waandishi wa habari za michezo kuacha dhana potofu ya kuripoti habari za uchochezi na badala yake waripoti zile  zinazoelimisha jamii.
Bendera alitoa kauli hiyo wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari za michezo  yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA yaliyomalizika mkoani Morogoro jana.
Mkuu huyo alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya waandishi wa habari   kuripoti  habari za migogoro jambo ambalo linachochea migogoro na kupelekea kushusha taaluma ya michezo hapa nchini.
Hali kadhalika hali hiyo imetolewa na  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego ambaye alifunga mafunzo hayo yaliyoshirikisha jumla ya waandishi 40 kutoka mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam, chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano  Vodacom Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wakati akifunga mafunzo hayo alisema waandishi wa michezo pia wanatakiwa kuacha ushabiki wa Simba na Yanga kitendo ambacho  kinachangia kupotosha sekta nzima ya uandishi wa habari za michezo.
 ‘’Nawaomba mzingatie mafunzo mliyopata ili kuboresha zaidi sekta ya habari za michezo,” alisema Dendego.
Alisema TASWA  imefanya jambo la muhimu kuandaa mafunzo hayo kitendo ambacho kimetoa changamoto  kwa wanahabari kuripoti habari zenye usahihi   tofauti na kukiripoti habari za ushabiki zaidi.
“Aliongeza kusema si kila siku  mnaegemea kuandika migogoro na habari ambazo hazina faida kwa mashabiki wa michezo wa Tanzania,  mnatakiwa kuandika habari za uhakika kutokana na kwamba  waandishi ni kioo cha jamii”. alisema
Alisema kutokana na mafunzo hayo, waandishi hao watakuwa wamekwiva vya kutosha na matunda yake anayategemea kuyaona watakavyorejea katika vyombo vyao vya habari.
Aliongeza kwa kuwashukuru wadhamini wa mafunzo hayo, kampuni ya simu za mkononi Vodacom na wadhamini washiriki kampuni ya mabasi ya Al Saedy  Bus Service kwa kujitolea kudhamini mafunzo hayo.
Ameahidi pia, kushirikiana na TASWA  bega kwa bega katika kuendeleza michezo  nchini, kwa sababu kuna mingine kama Mpira wavu na netiboli imedorora.
Kwa upande wa Vodacom kupitia Meneja Uhusiano na habari za Mtandao, Matina Nkurlu alisema,  kutokana na kampuni hiyo, kwa muda mrefu imekuwa mdau muhimu katika kuendeleza sekta ya michezo Kitaifa na Kimataifa nchini haikusita kudhamini mafunzo hayo.
‘’Vodacom imekuwa ikidhamini  michezo mbalimbali, kama Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Vodacom Miss Tanzania, Mwanza Cycle Challenge , Kilimanjaro Marathon na Mashindano ya mbio za mashua  za Vodacom Regata, imekuwa ikidhamini pia mafunzo ya kunoa waandishi wa habari kama ilivyofanya, alisema Matina.
Aliongeza kuwa: ‘’Pamoja na kufanya biashara bado tunaona ni muhimu kutoa mchango katika hii ili kuiwezesha Tanzania siku moja kuwa moja ya nchi zinazofanya  vizuri kwenye michezo kama tunavyosikia majina ya nchji za Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na nyingine.’’

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.