Habari za Punde

*TAIFA STARS YATUPWA NJE MICHUANO YA MCHUJO WA KUFUZU AFCON 2012, YAPIGWA 3-1 NA MOROCCO

Mshambuliaji wa timu ya Morocco, Mbark Boussoufa (kushoto) akiwatoka wachezaji wa Taifa Stars, Dan Mrwanda (katikati) na Juma Nyoso, wakati wa mchezo wa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika CAN2012 mjini Marrakech's Morocco usiku wa kuamkia leo. Morocco imeshinda 3-1 dhidi ya Tanzania.
************************************
Na Boniface Wambura, Marrakech Morocco
Timu ya Tanzania (Taifa Stars) usiku wa kuamkia leo imefungwa mabao 3-1 na Morocco na kundoshwa katika kinyang'anyiro hicho katika mechi ya mchujo kuwania tiketi ya AFCON 2012 iliyochezwakatika Uwanja wa Grand kushuhudia na maelfu ya watazamaji kwenye uwanja huo wenye viti 43,000.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1, ambapo wenyeji Morocco ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 19 kupitia kwa mshambuliaji wake, Marouane Chamakh kwa mpira wa kichwa ambao ulidunda kabla ya kumpita kipa Juma Kaseja wa Taifa Stars.
Katika dakika ya 40, Kiungo wa Stars Abdi Kassim aliisawazishia timu yake kwa shuti kali alilopiga umbali wa meta 35 lililomshinda kipa Nadir Lamyaghri kufuatia pasi ya Idrisa Rajab.
Mabao mengine ya Morocco ambayo imepata tiketi ya kucheza fainali za AFCON zitakazochezwa mwakani katika nchi za Equatorial Guinea na Gabon yalifungwa dakika ya 68 na Adel Taarabt.
Mbark alifuta matumaini ya Stars kupata sare katika mechi hiyo kwa bao lake la tatu alilifunga dakika ya 90 kwa shuti la chini akiwa ndani ya eneo la hatari.
Mwamuzi Bakary Gassema kutoka Gambia aliwaonya kwa kadi za njano Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Dan Mrwanda na Mohamed Rajab wa Stars wakati kwa upande wa Morocoo aliyeoneshwa kadi ya njano alikuwa nahodha wa timu hiyo Houcine Kharja.
Akizungumza baada ya pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen aliwataka wachezaji wake wasikate tamaa kutokana na matokeo hayo kwa vile walicheza na timu bora kuliko wao.
Alisema hivi sasa wanatakiwa kuelekeza akili kwenye mechi mbili zilizo mbele yao dhidi ya Chad.
Mechi hizo za mchujo kwa ajili ya kuingia hatua ya makundi ya mchujo Kanda ya Afrika kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwaka 2014 zitachezwa Novemba 11 mwaka huu jijini Ndjamena na Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars:- Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Nassoro Cholo, Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Dan Mrwanda, Henry Joseph, Mbwana Samata/John Bocco, Abdi Kassim na Mohamed Rajab/Mrisho Ngasa.
Morocco; Nadir Lamyaghri, Michael Basser, Abdelhamid El Kaoutari, Badri El Kaddouri, Mehdi Benatia, Younes Belhanda, Houcine Kharja, Mbark Boussoufa, Adel Taarabt/Youssef El Arabi, Marouane Chamakh/Said Fettah na Oussama Assaidi/Karim Al Ahmadi.
Taifa Stars inatarajiwa kurejea Dar es Salaam saa 2.30 asubuhi Oktoba 11 mwaka huu kwa ndege ya Qatar Airways.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.