Wafanyakazi wa boti ya Mistress wakiwa wamebeba samaki walizovua katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi yajulikanayo kama Latham Open yaliyoshirikisha nchi sita na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza (kulia) akitoa zawadi kwa mshindi wa uvuvi kwa upande wa watoto Kyle Balarin (15) aliyekuwa akitumia boti ya Tarka katika mashindano yaliyofanyika kisiwa cha Sinda mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Commodore Spiras Manoloudis wa Yatch Club akishuhudia utoaji wa zawadi hizo.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia) akimkabidhi zawadi Alfred Charles kwa niaba ya timu yake baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa upande wa boti ya Mistress katika mashindano yaliyofanyika huko Sinda kisiwani mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Kikundi cha Sanaa cha Jambo brothers kutoka Zanzibar kikionyesha sarakasi mbalimbali katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyokuwa yakiendelea kisiwani humo, ambayo pia yalidhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment