Habari za Punde

*WANANCHI WA KIJIJI CHA FRELIMO IRINGA WAMTAKA MBUNGE WAO KUANDAA MAANDAMANO KUSHINIKIZA HUDUMA YA MAJI

Wananchi wa Frelimo katika Manispaa ya Iringa siku ya tatu sasa wamekuwa wakitumia maji ya mto mchambawima ,mto ambao unatiririsha maji machafu kutoka katika vyoo na nyumba za wananchi wa Manispaa hiyo kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji safi katika Manispaa hiyo.
Kutokana na tatizo hilo wananchi wamemwomba mbunge wao, mchungaji Peter Simon Msigwa kuweza kuingilia kati na ikiwezekana kuandamana kama walivyowahi kufanya wananchi wa jimbo la Ubungo na mbunge wao Jonh Nyika,  hadi ofisi za idara ya maji ili kusaidiwa kero hiyo.
Wamesema kuwa tatizo la maji katika eneo hilo limeendelea kuwasumbua na baadhi wamekuwa wakilazimika kutafuta maji hayo katika mifereji ya maji machafu kwa ajili ya matumizi na kuhoji ukimya wa mamlaka ya maji safi na maji taka katika manispaa ya Iringa (IRUWASA) kuendelea kuwatesa wananchi hao bila ya kutoa matangazo yoyote juu ya tatizo hilo.
Imeandikwa na Francis Godwin Iringa

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.