Habari za Punde

*BFT NA TOC KUTOA MAFUNZO KWA WALIMU WA NGUMI TANZANIA

*MAFUNZO YA KIMATAIFA KWA WALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHAA  KIBAHA PWANI.

SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wameandaa mafunzo kwa walimu wa mchezo wa ngumi Tanzania.
Kozi hiyo itafanyika kuanzia tarehe 12-20 Nov 2011 Kibaha, Pwani katika shule ya Filbert Bayi.
Mkufunzi katika kozi hiyo ni kutoka Algeria,aliyeteuliwa na Chama cha ngumi cha Dunia (AIBA)
Jumla ya washiriki ni 30 wamechaguliwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kuja kuhudhuria mafunzo hayo, kwa kuzingatia mchango wao katika ushiriki wa matukio mbali mbali ya BFT hasa mashindano kwa kuleta timu au mikoa yao kama makocha na kujihusisha kikamilifu katika shughuri mbalimbali zinazohusu kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania
Zaidi makocha hao tayari walishapata mafunzo ya awali yaliyoandaliwa na BFT.
Baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo washiriki watakaofuzu watatambuliwa na kuingizwa katika data base za Chama cha ngumi cha Dunia [AIBA]
Pia wataweza kufundisha mchezo wa ngumi popote Duniani na kuruhusiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa kama makocha kwa mashindano yote yatakayo andaliwa kwa kufata sheria za AIBA.
Kwa uzoefu sisi kama BFT tunategemea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo,tunategemea kupata ushindani wa uhakika kutoka katika mikoa iliyopata nafasi ya ushiriki,na tunategemea kupata timu ya Taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa tofauti na awali ambapo wachezaji wengi walitokea DAR ES SALAAM na hasa katika vyombo vya ULINZI NA USALAMA.
Kwa msingi huo sasa tutategemea kupata ushiriki wenye tija katika mashindano mbalimbali ya kimataifa hasa kufuzu katika ushiriki wa timu yetu ya Tanzania katika mashindano ya Olimpiki 2012 London Uingereza.Na mashindano mengine ya kimatafa.
Makore Mashaga.
KATIBU MKUU BFT.
TEL 0713588818.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.