Habari za Punde

*BINADAMU ALIYEBADILKA NA KUWA JIWE MIAKA 500 ILIYOPITA

 Hadith, Hadith.... Hadith Njoo, Uongo Njoo, Utam kolea....Hapo zamani za kale miaka 500 iliyopita, babu zetu yaani watu wa kale wa miaka hiyo walikuwa ni watu waliokuwa na maumbo makubwa, warefu na wenye nguvu kuliko binadamu wote wa karne hii ya sasa.

Na watu hao walikuwa na imani za kweli ambapo mtu wa zamani alikuwa akiwa akikuambia kitu ama kukueleza juu ya jambo linaloweza kutokea baadaye basi jambo hilo litakuwa ama litatokea kweli baadaye.

 Jiwe hili kwa mujibu wa historia ya wakazi wa eneo la Gezaulole huko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, maeneo ya Kigamboni, alikuwa ni binadamu yaani mtu Mwanamama aliyekuwa amembeba mwanawe mgongoni akipita pembezoni mwa nyumba za makazi ya watu zilizokuwa zimejengwa pembezoni mwa Ufukwe wa Bahari ya Hindi, huku akijisuka nywele zake, inaana alikuwa kichwa wazi na eneo hilo palikuwa na Msikiti wa Ijumaa ambao ungali upo hadi hii leo na umebaki kuwa ni wa historia.

Eti imeelezwa Mama huyo akiwa na mwanawe mgongoni baada ya kufika eneo hilo ghafla aligeuka jiwe, ambalo lilikuwa na umbo na mwanadam aliyebeba mtoto na kuwafanya watu waliokuwapo eneo hilo kushikwa na butwaa huku kila mmoja akitimua mbio kutoa taarifa kwa familia yake na wazee wa Kijiji hicho.

Hivyo basi toka kutokea kwa tukio hilo Jiwe hilo limebaki katika eneo hilo ambalo zamani palikuwa ni karibu na nyumba za kuishi watu lakini kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi Jiwe hilo kwa sasa muda mwingine huwa liko ndani ya maji na muda mwingine huwa Nchi kavu kutokana na maji ya Bahari kupwa na kujaa yaani kuondoka na kurudi.

Na sasa eneo lilipo jiwe hilo limebaki kuwa ni eneo la Matambiko kwa wale wanaoamini Imani za Naniliu ambapo kila Wikiendi utakuta eneo hilo wamejaa jamaa zetu wa Kihindi na raia mbalimbali wakiendelea kutambika kwa kila mmoja na staili yake na kama unavyoona picha jiwe hilo likiwa limezungukwa na vitambaa vya kila rangi ambavyo huwekwa na wanadamu wanaofika kutambika katika jiwe hilo ambalo huitwa 'KIJIWE MTU'.
 Moja ya Kijimti kilichpo eneo hilo kikiwa na matambaa ya rangi ambayo yamewekwa na watu waliofika eneo hilo kwa lengo la kuabudu kwa imani zao na kutambika.
Picha hii ukiangalia kwa makini utaona watu kwa mbali Mke na Mume, wakiwa chini ya pango hili lililosheheni vitambaa vya rangi nyeupe na nyekundu, wakitambika na kuabudu kwa imani zao ama kwa kuagizwa na mganga wao kama walivyokutwa na kamera ya Sufianimafoto.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.