Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) akitoa tamko la kuwataka baadhi ya madaktari waliogoma kurudi kazini leo katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati alipokutana na kuzungumza na madaktari na kutoa tamko la kuwasimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Mutasiwa.
Baadhi madaktari wakifurahia Kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mkutano wao na katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Steven Ulimboka akitoa tamko la kurejea kazini kwa baadhi ya madaktari walioko katika mgomo kesho, mara baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuondoka.
Baadhi ya madaktari wakiwa katika mkutano wao wa kujadili kuhusu kurudi kazini mara baada ya Waziri Mkuu Mizengo kuondoka katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na madaktari leo baada ya kuwataka kurejea kazini ili kuwahudumia Watanzania katika Ukumbi wa mkutano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Watu mbalimbali wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati wa mkutano huo. Picha zote na Magreth Kinabo – MAELEZO
No comments:
Post a Comment