Kikosi cha Yanga.
*Yafuta wazo la kukata rufaa
Na Mwandishi wetu
KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imefuta wazo lake la kukata rufaa kwa Shirikisho la Kandanda Afrika (CAF) kupinga matokeo na vitendo vya ukiukwaji wa masharti waliyopewa ya kutocheza na mashabiki katika mechi yao ya marudiano dhidi ya timu ya Zamalek Sporting wiki iliyopita.
CAF ilitoa maelekezo kuwa katika mchezo huo, timu zote zinatakiwa kuingiza watu wasioidi 40, pamoja na Yanga kufuata sharti hilo, Zamalek ilikiuka na kujaza watu wapatao 400 ambazo walivalia mavazi ya kijeshi.
Askari hao walikuwa wakishangilia kwa nguvu timu hiyo, kitendo ambacho uongozi wa Yanga ilisema ni kinyume na utaratibu na kuweka nia ya kukata rufaa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Celestine alisema kuwa walichokifanya ni kuandika malalamiko kwa kamisaa wa mchezo huo tangu walipokuwa Misri na si kukata rufaa.
Mwesigwa alisema kuwa wameona kuwa uzito wa malalamiko yao hayatafuta matokeo ya mechi hiyo zaidi ya kuiongezea adhabu Zamalek ya kutocheza bila mashabiki.
Alisema kuwa hali hiyo itawafanya wao kupoteza fedha zao ambapo sasa wameamua kuwekeza nguvu zao zote katika kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na si vinginevyo.
“Tutapoteza muda na fedha kwa kukata rufaa, tumeona bora tuwekeza nguvu zetu kwenye ligi na wala si kwa kukata rufaa, malalamiko tuliyopeleka yanatosha,” alisema Mwesigwa.
Alisema kuwa kesi ya Simba SC dhidi ya Zamalek ni tofauti nay a kwao kwani wao walikuwa ya uhalali wa mchezaji na wala kikukwa kwa masharti ya kucheza mechi bila ya mashabiki.
No comments:
Post a Comment