Eneo hilo ndipo zilikuwa zimejengwa Nyumba za Kota kwa miaka mingi, ambalo kwa sasa zimebomolewa siku za hivi karibuni kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Kituo cha Mabasi ama Magari yaendayo kasi.
Sawa tumekuwa tukiona jitihada kufanikisha usafiri wa aina hii katika jiji la Dar es Salaam, ambalo limekuwa na karaa ya usafiri na hasa kutokana na Miundombinu mibovu iliwepo toka enzi zileeee, Na je iwapo vituo hivi vitajengwa na kukamilika vipi kuhusu njia ama barabara za magari hayo yatapita wapi ili kuweza kuendana na dhamira husika ya Mabasi yaendayo Kasi?
Kwani tumekuwa tukiona foleni zikitawala na kusumbua kila kona ya jiji hili kwa wenye magari tu mfano mzuri ni jana tu, je yakiongezeka mabasi hayo yatakuwa na njia zisizotumiwa na magari mengine ama ndiyo zitajengwa Barabara za juu?
Hili ni moja kati ya maswali ambayo yamekuwa yakiwasumbua wadau wengi wa mtandao huu na bila kupata majibu, ila Subira yavuta heri hivyo tusubiri tuone hadi vitakapokamilika vituo hivyo panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tukiwepo tutaona kilichokusudiwa ili kufanikisha hadhma hii.
Na je vipi kuhusu miundombinu ya barabara zetu itaimarishwa? na Kituo cha magari ya Mbagala na Temeke kitahamishiwa wapi? kwani hivi sasa imekuwa ni vurugu tupu katika eneo hili kutokana na magari kupakilia barabarani na huku mengine yakipata taabu kupita eneo hili.
No comments:
Post a Comment