Naibu Katibu Mkuu wa Maji, Binilith Mahenge.
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
NAIBU Waziri wa Maji, Binilith Mahenge ameziagiza bodi za Mamlaka ya Maji safi na Majitaka mijini kuwachukulia watumishi wote hatua zinazostahili , ambao wamesababisha mamlaka zilizopata hati zenye mashaka katika Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka hizo kwa mwaka fedha uliopita(2010/2011).
Kauli hiyo imetolewa leo(jana) na Naibu Waziri huyo wakati alipofungua mkutano mkuu wa 13 wa mamlaka hizo unaendelea kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku mbili umehusisha watu 200 ambao ni wakurugenzi, watalaamu wa wizara hiyo, TAMISEMI, Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa EWURA, DAWASA na DAWASCO na wadau wengine.
Mada kuu ya mkutano huo ni “Kuzijengea Mamlaka Uwezo wa Rasilimali watu katika Kutoa Huduma Endelevu”
“ Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka na ripoti zake ni kioo muhimu cha kupima uttendaji kazi, usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwenye mamlaka… Sikuridhika na kiwango cha kuongezeka mamlaka zilizopata hati zenye mashaka kutoka tatu mwaka 2009 /2010 hadi tano mwaka 2010/2011. Tegemeo langu mamlaka zote zipate hati safi ya ukaguzi wa hesabu.
Naibu Waziri Mahenge alizitaja mamlaka hizo kuwa ni Mtwara, Musoma, Songea, DAWASA na DAWASCO, ambapo alizitaka kuongeza nguvu katika usimamizi wa fedha katika mamlaka zao kwa kuhakikisha hesabu za mamlaka hizo zinatayarishwa kwa usahihi unaokubalika n kuondoa kasoro zilizojitokeza.
Aidha Mahenge aliongeza kuwa kasi ndogo ya utekelezaji wa program ya miradi ya maji iliyopangwa inachangiwa na uhaba wa fedha kwa kiasi kikukubwa na upungufu wa wataalamu wanaoweza kusimamia kwa makini utekelezaji wake kuanzia ngazi za mikoa , wialya, miji midogo na miradi ya kitaifa.
Aliyataja maeneo yenye upungufu kuwa ni usimamizi fedha za miradi, ununuzi, utoaji taarifa za utekelezaji wa miradi, ukusanyaji na utoji wa taarifa za miradi, uchambuaji na utunzaji takwimu.
Alisema hali hiyo inaonyesha umhimu wa kujenga uwezo kwa watendaji katika ngazi zote ili mapungufu yaliyopo yasiendelee kuonekana, hivyo alizitaka bodi hizo kuwa na mipango ya mafunzo inayotekelezeka na kulenga mapungufu hayo.
Mahenge alisema changamoto nyingine katika utkelezaji wa program ya maendele ya sekta ya maji ni kuchelewa kwa fedha za maendeleo kutoka wadau wa maendeleo, hali ambyo imesababisha wakandarasi kupunguza kasi ya ujenzi na kutoza riba, ikiwemo kuchelewa kukamilika kwa ujenzi.
Alisema uchelewaji wa malipo unatokana na hasa na uchelewashaji wa taarifa za utekelezaji kutokakwa watekelezaji wa ngazi zote. Hivyo hadi kufikia Aprili mwaka huu jumla ya sh. bilioni 32.7 hajijalipwa kati ya hizo fedha za wakandarasi ni sh. bilioni 30.1 na wahandisi washauri ni sh. bilioni 2.6.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhadisi Christopher Sayi alisema katika jiji la Dares Salaam na maeneo yanayohudumiwa na DAWASCO, kiwango cha utaoji wa huduma ya majisafi kimeshuka na kufikia asilimi 51kipindi cha mwezi Juni,2011 kutoka asilimia 55 ya Juni 2010.
Alisema upungufu huo umetokana na kupungua kwa uzalishajimaji uliosababishwa na mgao wa umeme na ongezeko la maeneo ya utoaji huduma kwa kupanuka kwa jiji.

No comments:
Post a Comment