Mkali wa miondoko ya Pwani kutoka Zanzibar AT akishambulia jukwaa  sambamba na wanenguaji wake wakati wa tamasha la Washindi wa Tuzo za Kilimanjaro “Kili Music Award Winners Tour” lililofanyika katika uwanja wa Umoja mjini Mtwara. 
Mkongwe wa Taarab, Bi Hadija Kopa akitumbuiza jukwaani na kukonga nyoyo za wakazi wa Mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi Mkoani Mtwara kwa vibao vyake kadhaa ambavyo vimempa tuzo ya Kili Music Award 2012
Show ya wakali wa Kili Music Award 2012 ndani ya Uwanja wa Umoja mjini Mtwara ndio imeanza sasa. Pichani ni Mshindi kutoka Mtwara ambaye ataenda kurecord jijini Dar es Salaam Nicolazo akitumbuiza na kuwashinda wenzake wawili.
Chipukizi wa 3 wa Mtwara waliokuwa wakichuna kutafuta mmoja atakaeenda Kurecord jijini Dar es Salaam kwa udhimi wa Kilimanjaro Lager
Mashabiki wakifuatilia show hiyo ya kutafuta vipaji.

Shangwe za kumshangilia Chipukizi ambaye ni kipaji kipya cha Kili Music Award kutoka Mtwara: Picha na Father Kidevu