Mabondia, Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa pambano lao linalotarajia kufanyika Siku ya Saba Saba katika uwanja mpya wa Taifla .Picha na Maktaba
***********************************
WASANII wa Filamu nchini 'Bongo Movie', wanatarajia kukipiga na wasanii wa Bongo Flava, katika mchezo wa Soka, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, siku ya pambano la ngumi la Francis Cheka na Japhet Kaseba, pambano ambalo pia litasindikizwa na msanii wa miondoko ya Bongo Flava, Diamond.
Mbali na burudani hiyo ya soka na Diamond, pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali nchini, pamoja na mapambano ya utangulizi.
Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju, amesema kuwa maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vizuri na kuwataka mashabiki wa ngumi kufika kwa wingi kushuhudia mawe na kuwaomba radhi kutokana na upotoshwa wa baadhi ya watu waliokuwa wakitangaza tofauti kuhusu pambano hilo.
''Maandalizi yote yanaendelea vizuri na zile longolongo zilizokuwa zikitangazwa tofauti na baadhi ya watu kuhusu pambano la wakali hawa tumekwishasawazisha kwani wao walikuwa wakitangaza bila kufanya mazungumzo na mabondia wala huyo waliekuwa wakimtangaza kuwa eti, angekuja kuzichapa na Cheka, hakuna kitu kama hicho, pambano letu la Cheka na Kaseba lipo palepale kama kawa''. alisema Kaike.
Kaike, aliwataja baadhi ya mabondia watakaosindikiza pambano hilo ni pamoja na Adiphoce Mchumiatumbo, atakayezichapa na Ramadhani Kido, wakati Amos Mwamakula ataonyeshana kazi na Rashini Ali, na Mkongo Kanda Kabongo, akizipiga na Said Mbelwa na bondia chipukizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala chini ya Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli 'Masta' na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba.
No comments:
Post a Comment