Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa kanda ya ziwa mwaka 2012.
Mashindano hayo ya kupiga kasia, yanayo dhaminiwa na bia ya “Balimi Extra Lager” yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara na visiwa vya Ukerewe. Mashindano haya yamekuwa yakijizolea umaarufu katika kanda ya ziwa mwaka hadi mwaka na yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka kila mwaka.
Akiongelea mashindano ya mwaka huu wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Edith Bebwa alisema, Ni zaidi ya miaka saba sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki Balimi imefanikiwa kuleta changamoto kubwa katika mchezo wa kupiga makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika.
Kwa hivi sasa timu zote zimeshaanza maandalizi, tayari kwa mashindano ya ngazi ya mkoa ambapo kwa mwaka huu yataanzia Kigoma tarehe 20 Octoba, ikifuatiwa na Kagera tarehe 27 Octoba, Mwanza tarehe 4 Novemba, Kisiwa cha Ukerewe tarehe 10 Novemba na Mara tarehe 17 Novemba. Baada ya fainali hizo za ngazi ya mikoa timu zilizoshinda zitakutana katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza tarehe 2 Desemba pale Mwaloni Kirumba.
Akizungumzia timu zitakazofuzu kuingia fainali kuu, Bi Edith alisema; timu tatu za wanaume na mbili za wanawake zitakazoshika nafasi za juu zaidi katika ngazi ya mkoa ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza.
Na timu zilizochukuwa ubingwa mwaka jana upande wa wanaume na wanawake watapata fursa ya moja kwa moja ya kuingia finali kuu za mwaka huu ili kutetea ubingwa wao.
Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za Mkoa na fainali kuu, Meneja Masoko Bw. Fimbo Butallah alisema; Kama ilivyo ada, zawadi zimekuwa zikiongezeka kila mwaka, ukiwemo mwaka huu 2012, ambapo zawadi zimepangwa kama ifuatavyo;
Ngazi ya Mikoa
|
Fainali Kuu
| ||||
Wanaume
|
Wanawake
|
Wanaume
|
Wanawake
| ||
Mshindi wa kwanza
|
900,000
|
700,000
|
2,700,000
|
2,300,000
| |
Mshindi wa Pili
|
700,000
|
600,000
|
2,300,000
|
1,700,000
| |
Mshindi wa Tatu
|
500,000
|
400,000
|
1,700,000
|
900,000
| |
Mashindi wa Nne
|
400,000
|
300,000
|
900,000
|
700,000
| |
5 hadi 10 - Kila timu
|
250,000
|
200,000
|
500,000
|
250,000
|
''Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki. Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya yenye mvuto na msisimko wa aina yake''.
No comments:
Post a Comment