Habari za Punde

*KESI YA SHEIKH PONDA YAAHIRISHWA HADI MEI 9 MWAKA HUU

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa tatu kulia) akiwa na mshtakiwa mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea  kupanda basi la magereza kureje rumande baada ya hukumu ya kesi yao kuahirishwa hadi Mei 9. Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiliwa na makosa matano ya kula njama na kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T, uliopo Markaz Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Sh. milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akipanda basi la magereza.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.