Maelfu ya wananchi na waumini wa dini ya kiislamu waliofurika katika msikiti wa Mwembeshauri katika maziko ya Marehemu Bikidude leo, wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa marehemu huyo wakati wakielekea mazikoni kijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati Unguja.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika maziko ya marehemu Bi Fatma Baraka 'Kidude' kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Msanii mkongwe wa Muziki wa Mwambao (Taarab) Tanzania,Marehemu Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo mchana.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kuli) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia waliokaa) Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif, na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,wakiomba dua baada ya maziko ya Msanii maarufu Fatma Binti Baraka 'Kidude' aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Kati Unguja.
No comments:
Post a Comment