Habari za Punde

*SHY-ROSE BHANJI AGALAGAZWA NA ANNA KIBIRA UCHAGUZI WA CHANETA


Aliyekuwa mjumbe na baadaye Katibu mkuu wa CHANETA Anna Kibira, amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa pete chaneta Katika uchaguzi uliofanyika leo, Mkoani Dodoma, uliosimamiwa na mkuu wa wilaya ya Bahi na Betty Mkwasa .
 
Katika uchaguzi huo Anna Kibira,  amemgalagaza mpinzani wake Shy-Rose Bhanji, kwa tofauti ya  la kura arobaini (40) katika nafasi ya uenyekiti, ambapo Anna Kibira amenyakua jumla ya kura 61 dhidi ya Shy-Rose Bhanji aliyeibuka na kura arobaini na moja tu.
 
Nafasi mbalimbali zilikuwa zikigombewa katika chama hicho cha mpira wa pete ambapo kulikuwa na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao walikuwa wagombea tisa lakini wamepatikana wagombea sita  tu.

Grace Khatib, ambaye alikuwa hana mpinzani katika nafasi ya mweka hazina alipata kura za ndio 66 na kura za hapana 16 kati ya kura 82 zilizopigwa.

Katika nafasi ya makamu mwenyekiti kulikuwa na wagombea wawili Zainab Mbiro na Agnes Madasila katika nafasi hiyo Zainabu Mbiro alipata kura hamsini saba wakati mpinzani wake amepata kura 27
 
Kwa maana hii CHANETA imepata safu mpya kabisa ya uongozi baada ya ile ya mwanzo ile kuamua kuachia ngazi na wagombea wengine kuamua kutokugombea kabisa uongozi katika chama hicho cha mchezo wa pete kwani safu mpya inatakiwa kufanya kazi ya ziada kufikia malengo ya kuinua mchezo wa mpira wa pete kwani uongozi uliopita uliiwezesha CHANETA kuifikisha timu ya taifa ya mchezo huo katika mashindano ya dunia.   
 
Chama kiliweza kuaandaa michuano ya mataifa ya afrika ni wazi kabisa wanachangamoto kubwa ya kufanya japokuwa mara baada ya ushindi kibira amesema kuwa anataka kuupeleka mchezo huo mikoani na kwenda kuuimarisha zaidi vijijini .    

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.