Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, akizungumza wakati akifungua rasmi semina kuhusu Changamoto zinazowakabiri Maalbino kwa waheshimiwa wabunge katika Ukumbi wa Msekwa, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa Legislative Support Project, imeandaa semina ya kuwapa Uelewa waheshimwa Wabunge kuhusu Changamoto zinazowakabiri Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albinism) ili kuwa na uwelewa mpana kuhusu changamoto zinazowakabili albino.
Semina hii ni mwendelezo wa semina za kutoa elimu kwa waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Ofisi ya Bunge kupitia Mradi wa Legislative Support Project, ambao upo chini ya Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) ili kuwajengea wabunge na watumishi katika kutekeleza majukumu yao ya Kibunge, hususani, uwakilishi wa wananchi pamoja na kuisimamia na kuishauri serikali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Margareth Sitta (MB) akitoa neno la Utangulizi wakati wa Ufunguzi wa Semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifafanua baadhi ya changamoto zinazowakabiri maalbino kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kufungua rasmi Semina hiyo.
Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Mbunge wa Lindi Mjini Mhe. Salum Barwani ambaye nae ni mlemavu wa ngozi akitambulishwa katika semina hiyo.
No comments:
Post a Comment