Habari za Punde

*MSHINDI WA MIL 100 WA PROMOSHENI YA VODACOM MAHELA AFUNGUA AKAUNTI NMB

Benki ya NMB, imemkaribisha  mshindi wa milioni 100 wa Vodacom MAHELA , Bwana  Valerian Nickodemus, kwa kumfungulia akaunti na kujitolea na kumpa mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya fedha  ili kumwezesha kuwa na matumizi yenye tija katika maisha yake, kupitia fedha hizo alizojishindia.
Mshindi wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw. Valerian Nickodemus (katikati) akifurahia 'Mahela' pamoja na  Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na  Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twisa, baada ya kukabidhiwa fedha hizo, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mshindi wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw. Valerian Nickodemus (katikati) akikabidhiwa kadi yake ya NMB ATM na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) baada ya kufungua akaunti katika benki ya NMB. Kushotoni ni Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom,  Kelvin Twisa, akishuhudia.
Mshindi wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw. Valerian Nickodemus (katikati) akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) baada ya kufungua akaunti katika benki ya NMB. Kushoto ni Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom,  Kelvin Twisa, akishuhudia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.