Habari za Punde

*BAADA YA JITIHADA ZA MWAKYEMBE, MATUNDA YAANZA KUONEKANA, MWAMKE MNAIGERIA ANASWA NA MADAWA UWANJA YA KULEVYA WA NDEGE

Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Anthonia Ojo (25) Raia wa Nigeria amenaswa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, jana akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya.Mwanamke huyo alikuwa safarini akielekea Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways. Mwanamke huyo aliingia nchini Agosti 30 akitokea Nigeria. 

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, ambaye alisema kuwa, Ojo anaendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwa ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye taratibu nyingine za kumfikisha Mahakamani. 
Anthonia Ojo, akiwasili kwenye Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege baada ya kukamatwa.
Paspoti ya Mwanamke huyo kama inavyosomeka.
Begi lake lenye mzigo likiingizwa kituoni kukaguliwa....
Mtuhumiwa huyo baada ya ukaguzi alianza kuzitoa dawa hizo katika vijimkebe vya Poda na Shampoo.
Akiendelea kumimina dawa hizo......
Sehemu ya mzigo huo.....
Kumbukumbu za kusafiri kwa mwanamke huyo zinaonyesha kuwa alishawahi kuja jijini Dar mwaka 2011. Chanzo Robert Okanda

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.