![]() | ||||
| Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu utata wa vifaa vya kieletronik vya kutoa risiti(EFD) |
***********************************************
Na Magreth Kinabo
Serikali imesema imeshaelekeza wasambazaji wa vifaa vya eletroniki vya kutoa risiti (EFD) kuuzwa
kwa bei tofauti kulingana na
ubora wake.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa
Fedha Saada Mkuya Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye
ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri
huyo ,alitoa ufafanuzi huo baada
kuulizwa swali na waandishi wa habari kufutia mgomo wa wafanyabiashara
unaoendelea katika baadhi ya mikoa kufutia kifaa hicho kuuzwa kwa bei ya Sh. 700,000
na 800,000 ambayo wanadai ghali.
“ Utumiaji wa EFD si kumkomoa mfanyabiashara bali ni
kuongeza mapato ya Serikali katika kuendeleza maendeleo ya nchi".
Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo alisema vifaa hivyo vipo
vinavyouzwa kuanzia bei ya 100,000 na kuendelea,hivyo na kuwataka wasambazaji
kuuza vifaa hivyo kulingana na bei iliyopangwa kulingana na ubora.

No comments:
Post a Comment