Frank
Mvungi-Maelezo
Wabunge
wanaowakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wamempongeza Rais
Jakaya Kikwete kufuatia hotuba yake aliyoitoa Bungeni Dodoma tarehe 07/11/2013
kuhusu Mustakabali wa Jumuiya Hiyo.
Hayo yalisemwa
na Mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Adam Kimbisa wakati wa mkutano na waandishi wa
habari jana jijini Dar es salaam.
Mh. Kimbisa
alisema wabunge hao wanampongeza Mh. Rais kwa kuchukua fursa ya kuongea na
Watanzania kupitia Bunge na kueleza masuala kadhaa baina ya Nchi wanachama na
hali ya hivi sasa ndani ya Jumuiya.
Alifafanua zaidi
Mh. Kimbisa alisemaMh. Rais amefanya uchambuzi wa kina kuhusu matatizo
yaliyoikumba jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia mikutano mitatu iliyofanywa
na nchi tatu za Kenya,Uganda na Rwanda ikiwatenga Tanzania na Burundi.
Alieleza zaidi
kuwa wabunge wa bunge hilo wanaungana na Watanzania wengi kuhusu kuwepo kwa
shirikisho la Afrika Mashariki lakini wanataka hatua hiyo isifanywe haraka bali
kwa umakini mkubwa,sera ambayo pia Serikali ya Tanzania imeipa kipaumbele.
Pia alisema
jambo la msingi ambalo mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya umesema ni kuwa
Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi kwa manufaa ya wananchi na isiwe ya viongozi
ambapo wananchi watashirikishwa katika kila hatua na kila ngazi ili waweze
kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao.
Katika hatua
nyingine wabunge hao waliipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua kwa
kuwarejesha makwao wahamiaji haramu kutoka Burundi,Rwanda,Uganda,DRC nchi nyingine ambao walitishia na kuharibu hali ya
usalama na mazingira katika maeneo ya Mikoa ya Kagera,Geita na Kigoma.
Aidha wabunge
hao wameiomba Serikali iendelee kusimamia suala hilo kwani baadhi ya wahamiaji
haramu wameanza kurejea katika maeneo husika na wananchi wameanza kutoa
malalamiko dhidi ya wahamiaji haramu.
No comments:
Post a Comment