Habari za Punde

*YANGA YAMALIZA MZUNGUKO WA KWANZA IKIWA KILELENI, AZAM,MBEYA CITY ZAGAWANA POINTI

Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' akimzuia mshambuliaji wa JKT Oljoro,wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeendeleza utaratibu wake wa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambapo na leo imeweza kushinda kwa idadi hiyo ya mabao.
***************************
Golikipa wa Mbeya City, akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake, wakati wa mchezo dhidi yao na Azam Fc, uliochezwa kwenye uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare kwa kufungana mabao 3-3, ambapo Mbeya City walikuwa wakiongoza na Azam walifanikiwa kusawazisha katika dakika za mwisho, kupitia kwa Hamis Mcha.
***********************************
KATIKA mchezo wa leo, Yanga walikuwa wakihitaji ushindi katika mchezo wao dhidi ya Oljoro huku hesabu za viongozi, mashabiki wa timu hiyo, zikitaka mchezo kati ya Mbeya City na Azam uliochezwa Chamanzi umalizike kwa sare ili timu hizo ziweze kugawana pointi na kuiachia nafasi ya kwanza na hayo ndiyo yaliyotokea katika mchezo huo, ambapo Yanga wamekalia Usukani wa Ligi hiyo kwa kuwa na jumla ya pointi 28.
Mabao hayo matatu yaliyofungwa na Simon Msuva dakika ya 23 na Mrisho Ngassa dakika ya 30 na lile la tatu lililofungwa na Jerry Tegete yalitosha kuifanya Yanga imalize mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni baada ya kutimiza pointi 28 baada ya kucheza michezo 13. 
Katika mchezo wa Chamanzi Azam walilazimisha sare dhidi ya Mbeya City kwa kufungana mabao 3-3 na kuifungulia njia Yanga kukaa kileleni baada ya kuwazidi kwa pointi mbili.
Azam na Mbeya City ambao walikuwa kileleni kwa pointi 26 na sare hiyo timu zote sasa zimefikisha pointi 27 kila moja huku Azam wakiwa nafasi ya pili wakati kwa tofauti ya magoli ya kufunga na Mbeya City inarudi nafasi ya tatu kwa tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.
Nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo inashikiliwa na Simba wenye pointi 24 baada ya kushinda mchezo wake wa jana dhidi ya Ashanti United.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.