Habari za Punde

*YANGA YAVUNJA MIIKO YA 3-0, YAKAA KILELENI BAADA YA KUICHAPA JKT RUVU MABAO 4-0

 Mshambuliaji wa Yanga, aliyeingia kuchukua nafasi ya Didier Kavumbagu, Jerry Tegete, akimtoka beki wa JKT Ruvu, Nashon Naftal, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Katika mchezo huo Yanga imeshinda mabao 4-0, mabao mawili yakifungwa na Mrisho Ngasa, katika dakika za 4 na 23 kipindi cha kwanza, bao la tatu limefungwa na Oscra Joshuo, katika dakika ya 50 na bao la nne limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 86. 

Kwa matokeo hayo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 25 na kukaa kileleni mwa ligi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Azam Fc, ikifuatiwa na Mbeya City, zenye pointi sawa 23 kila moja, huku watani wao wa jadi wakibakia katika nafasi ya nne wakiwa na Pointi 21.
 Jerry Tegete (kushoto) akishangilia bao lake kwa staili ya kunong'oneza, huku akipongezwa na Simon Msuva (kulia) na Mrisho Ngasa.
 Didier Kavumbagu, akimfinya beki wa JKT Ruvu Mussa Zubery, wakati wa mtanange huo.
 Simon Msuva (kulia) akiruka daruga la beki wa JKT Ruvu na kuambaa na mpira, ambapo alifanikiwa kutoa pasi nzuri iliyomkuta Hamis Kiiza, aliyeshindwa kupata bao la wazi.
 Sehemu ya Jukwaa la mashabiki wa Simba, likiwa tupu, haikuweza kufahamika sababu za kutohudhuria kama ilivyokuwa katika mechi za siku za nyuma.
 Mashabiki wa Yanga, ilikuwa ni shangwe......
 Hamis Kiiza, akipiga mpira wa kichwa na kusababisha heka heka langoni mwa JKT Ruvu.
Mrisho Ngasa, akiwafinya mabeki wa JKT Ruvu.....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.