Habari za Punde

*AZAM FC KIBARUANI KESHO UGENINI KWA 'WAMAKONDE' KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Mshambuliaji wa Azam Fc, Kipre Tchetche (katikati) akiwa kazini.
****************************************
Na Sufianimafoto Reporter, Dar
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam Fc, kesho watakuwa na kibarua kigumu watakaposhuka dimbani ugenini kukipiga na timu ya Ferrovirio De Beira katika mchezo wa marudiano  wa Raundi ya awali.

Akizungumzia mchezo huo Msemaji, ambaye ni Ofisa Habari wa  wa Azam Fc, Jafari Iddi, alisema kuwa timu yao inaimani na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano na kuweza kusonga mbele.

Aidha Jafari, alisema kuwa Kikosi chao kipo kamili na hakuna majeruhi hata mmoja,  na kuongeza kuwa ni lazima 'Wamakonde wachinjiwe nyumbani kwao'.

''Kama mungu akipenda kesho tukaamka salama, basi Wamakonde waandike maumivu kwani tutawafunga tena, kwani tupo fiti kwa asilimia 100''. alisema Iddi.

Baada ya matokeo ya ushindi wa bao 1-0 nyumbani katika mchezo uliopita timu ya Azam Fc sasa itahitaji sare yeyote ili iweze kusonga mbele katika michuano hiyo. 

Kinachotakiwa ni juhudi za washambuliaji wa Azam, waweze kupata bao la ugenini tu, kwani hata kama wakifungwa 2-1 au 3-2 au kwa tofauti yeyote ya bao moja ilimradi nao kupata bao, basi Azam itasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.