Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho, Azam FC leo imeshindwa kujitetea mbele ya wamakonde timu ya Ferroviario kwa kukubari kipigo cha mabao 2-0.
Azam imefungwa na wenyeji Ferroviario de Beira katika mchezo uliochezwa mjini Beira Msumbiji kwenye mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho Afrika.
Kws matokeo hayo sasa Azam imeondolewa kwenye michuano hiyo. Matokeo hayo yanaifanya Azam itolewe kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya awali kushinda bao 1-0 mjini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment