Chargé d'Affaires, a.i. Virginia M. Blaser (left) presents the 2014 Tanzanian Woman of Courage award upon Community Health and Gender-Based Violence Activist Joyce Stephano Nyembe (right) during a ceremony at the United States Chief of Mission’s residence in Dar es Salaam on March 26. Ms. Nyembe was honored for her perseverance and leadership fighting for the rights of women and children, and especially those living with HIV and AIDS, and victims of gender-based violence. She is the eighth recipient of the Tanzanian Woman of Courage Award since the U.S. Embassy began this recognition in 2008.
****************************
Hotuba ya Kaimu Balozi Virginia M. Blaser,
Kwenye hafla ya Kutunuku Tuzo ya Mwanake Jasiri wa Kitanzania kwa Mwaka 2014
Iliyofanyika Jumatano, 26 Machi 2014 Nyumbani kwa Balozi Waheshimiwa,
Bi. Joyce Stephano Nyembe, Mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri kwa Mwaka 2014, Bi. Anna Maembe, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Merina Njelekela, Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili na Mshindi wa Tuzo ya Haki ya Dkt. Martin Luther King kwa Mwaka 2010.
Bi. Maimuna Kanyamala, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake la Kivulini la jijini Mwanza na Mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri wa Mwaka 2011.
Ndugu, jamaa na marafiki wa Bi. Nyembe;
Wanawake mashuhuri mliokusanyika hapa mchana wa leo;
Itifaki imezingatiwa.
Habari za mchana?
Karibuni.
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wote nikiona fahari kuwa miongoni mwa wanawake mahiri waliokusanyika hapa mchana wa leo. Hebu geuka na mwangalie mwanamke aliye kulia na kushoto kwako.
Tumewaalika hapa hivi leo kutokana na mchango wenu mkubwa katika kuwajengea uwezo wanawake kutoka Nyanja zote za jamii nchini kote Tanzania.
Ukiwaangalia washiriki kutoka Ubalozi wa Marekani pekee, utaona kuwa wote ni wakuu wa Taasisi – USAID, CDC na vitengo ya ubalozi, ubalozi unaosimamia msaada rasmi kwa Tanzania wa Zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 750 kwa mwaka.
Sehemu kubwa ya fedha hizo zikielekezwa katika sekta ya afya, sekta ambayo mshindi wa tuzo yetu ya leo anajihusisha nayo kwa karibu sana.
Uwakilishi huu mkubwa wa wanawake si hapa tu bali pia katika Wizara ya Mambo ya Nje huko Washington, ambapo kwa mara ya kwanza katika historia, watano kati ya Mawaziri Wasaidizi sita wanaosimamia maeneo mbalimbali ya kijiografia ni wanawake, ikiwa ni pamoja na Waziri Mdogo anayeshughulikia masuala ya Afrika.
Hakika hiki ni kipindi cha kusisimua sana katika historia yetu ambapo wanawake wapo mstari wa mbele katika uandaaji wa sera, wakileta mtazamo wa kipekee katika ufanyaji maamuzi ya kisera yanayogusa jamii yote.
Lakini kila mmoja wetu hapa anaweza kabisa kuwa na mchango muhimu katika maamuzi ya kisera yanayofanywa katika kila ngazi. Na hivyo ndivyo mshindi wa tuzo yetu, Bi. Joyce Stephano alivyofanya.

Tupo hapa kutambua michango ya mwanamke ambaye vitendo vyake vinaelezea maana halisi ya kuwa mtu jasiri. Mwezi Machi kila mwaka, toka mwaka 2008, Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam umekuwa ukitambua na kuenzi jitihada za wanawake jasiri wa Kitanzania katika kuendeleza haki za wanawake.
Kipindi hicho pia ubalozi huadhimisha Mwezi wa Historia ya Wanawake. Baada ya kupitia majina ya wanawake wengi jasiri kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania, tulimchagua mwanamke anayeishi na kuendesha shughuli zake za kila siku kwa ujasiri jijini Mwanza – yeye ni mwanaharakati wa afya ya jamii, kiongozi, mwalimu na mjasiriamali mdogo Joyce Stephano Nyembe.

Kwa ruhusa yenu, naomba nitoe maelezo mafupi kuhusu Bi. Nyembe na malengo yake maishani. Lakini kabla sijafanya hivyo, najua wengi wenu tayari mnamfahamu Bi. Nyembe na wanawake wengine kama yeye ambao wanaongoza nchi, biashara na kulea watoto.
Tunafahamu fika kwamba ni mama zetu, wake zetu na binti zetu ndio wanaofanikisha mambo mengi katika jamii zetu. Mathalan, katika kukabiliana na janga la UKIMWI, ni akina mama ndio kwa kiwango kikubwa hubeba jukumu la kuwahudumia wagonjwa.
Ni wanawake ndio hutunza familia na jamii na ni wanawake ndio wanaowahudumia wale walio wanyonge zaidi katika jamii zetu. Ni kwa sababu hiyo tumemchagua Bi. Nyembe kuwa mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Jasiri wa mwaka huu kwa kazi yake ya kuboresha maisha ya Watanzania wanaoishi na VVU na UKIMWI na hasa baada ya yeye mwenyewe kuwa mwathiriwa wa miaka mingi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Pamoja na kuwa na mwanzo mgumu akitokea katika hali duni, Bi. Nyembe ameweza kuvumilia na kuhimili mikikimikiki mingi na kuweza kuwa mfano wa kuigwa na mwanaharakati katika jamii yake. Akifahamika zaidi katika jamii yake kama “Mama Mshauri,” uzoefu wa kiuongozi wa Bi. Nyembe ulianza mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya msingi.
Alianza kwa kufundisha madarasa ya elimu ya watu wazima akifundisha masomo ya darasa la tatu hususan kwa wanawake. Madarasa yake yalipata umaarufu sana na wanafunzi wake walifanya vizuri sana katika mitihani yao ya taifa kiasi cha kupewa cheti na serikali kama Mwalimu Bora wa Elimu ya Watu Wazima Tanzania. Wakati huo huo alipewa cheti kinachomuwezesha kufundisha katika mkoa wowote hapa nchini.

Akitambua mapenzi na kipaji chake katika ufundishaji katika jamii, Bi. Nyembe alianza kujihusisha kikamilifu katika kazi za kuhudumia jamii. Alijiunga na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake la Kivulini ambalo lilimpatia fursa nyingi za kielimu na uongozi wa jamii. Kuanzia hapo alianza kufanya kazi na watu wote wa jamii yake – wanaume, wanawake na vijana – ili kuinua hali ya maisha ya wanawake na wasichana.
Bi. Nyembe amewasaidia moja kwa moja zaidi ya watoto 40 kwa kuwaondoa katika mazingira ya unyanyasaji na ukandamizwaji au kwa kuzielimisha familia zao. Aidha, amewasaidia mamia ya watu wengine kwa kupitia shughuli za uanaharakati wa kijamii. Hivi sasa nyumbani kwake anaishi na kuwatunza watoto yatima watano ambao hapo awali walikuwa wametelekezwa na wakiishi katika mazingira magumu.
Hakika wanawake ndio wanaofanikisha mambo mengi, lakini si wakati wote ambapo Wanawake wanafanikishiwa mambo yao. Wanawake wanakabiliwa na aina nyingi za ubaguzi. Wanawake ndio hukabiliwa zaidi na uwezekano wa vitendo vya ukatili vinavyofanywa na wenza wao na wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa VVU.
Hali kadhalika, katika jamii nyingi wanawake hutengwa na kutokushirikishwa katika mambo mbalimbali hususan yahusuyo ufanyaji wa maamuzi.
Kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti UKIMWI, mmoja kati ya kila wanawake watatu amewahi kufanyiwa au atafanyiwa ukatili wa kimwili na kijinsia na mwenza wake katika kipindi fulani cha maisha yake. Aidha, takwimu hizo zinaonyesha kuwa katika kila saa moja wanawake vijana wapatao 50 wanapata maambukizi mapya ya VVU.

Lakini Joyce Nyembe ni mpambanaji; ni mwanamke anayetaka kuwahamasisha na kuwatia moyo wengine katika jamii yake kupinga na kupiga vita desturi zinazokubalika kitamaduni lakini zenye madhara makubwa kijamii.
Yeye mwenyewe akiwa ni mwathiriwa wa vitendo vya ukatili majumbani, Joyce anafahamu vyema athari mbaya za vitendo hivyo na jinsi ambayo jamii inakubali na kufumbia macho ukatili dhidi ya wanawake. Hata hivyo amekataa kuvunjwa nguvu na vitendo hivyo au kukatishwa tamaa na takwimu, hadhi yake na hali yake. Inahitaji mtu jasiri kufanya hivyo.

Bi. Nyembe alianza kuelimisha jamii yake jinsi ya kuzuia ukatili wa majumbani. Ameshinda changamoto binafsi na historia yake mwenyewe ya kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuweza kujenga ufahamu wa jamii katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo.
Mbali na shughuli za kupigania haki katika jamii yake, amekuwa akishiriki pia katika kampeni ya kimataifa za kupiga vita ukatili wa majumbani, iitwayo “We Can” (Tunaweza).
Kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kama vile radio, magazeti na televisheni pamoja na filamu fupi iitwayo “Raising Voices SASA!” (Paza Sauti Sasa) tutakayoiona hivi punde, Bi. Nyembe amezungumza katika ngazi ya kimataifa.

Kwa kupitia kazi zake za kila siku za kupigania haki ya jamii ya kiafya na uongozi katika jitihada za kukabiliana na janga la VVU na UKIMWI, Bi. Nyembe amekuwa ni ushuhuda hai; mtu anayewatia moyo wanawake wengine waishi maisha yao bila kufungwa na hali zao iwe ni za kiafya, kielimu au kijamii.
Toka alipogunduliwa kuwa anaishi na VVU, amekuwa akitoa elimu kwa watu wengine katika jamii yake kuhusu umuhimu wa kupima VVU, kujitangaza, kujilinda na kuwalinda wengine. Kutokana na jitihada zake kubwa za kukabiliana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoisha na VVU/UKIMWI katika jamii yake, Bi. Joyce Stephano Nyembe ameweza kuleta mabadiliko aliyotaka kuyaona katika dunia inayomzunguka.

Kwa hakika huu ndio ujasiri. Kufanya kazi pale ulipo ili kuleta mabadiliko chanya bila kujali vikwazo vinavyokukabili. Hivyo ninatoa wito kwa kila mwanamke aliyehudhuria katika hafla hii, pale tutakapokuwa tumeketi kwa ajili ya kupata chakula cha mchana, tutumie fursa hiyo kujadili ni kwa namna gani sisi kama viongozi wa kijamii wanawake kutoka serikalini, sekta binafsi na mashirika ya kimataifa tunaweza kuendeleza kazi ambayo Bi. Nyembe ameianza katika kuboresha jamii nchini Tanzania.
Napenda sasa kumkaribisha jukwaani Bi. Joyce Stephano Nyembe.
Bi. Nyembe, ninakutunukia Tuzo ya Mwanamke Jasiri ya Mwaka 2014 itolewayo na Ubalozi wa Marekani, jijini Dar es Salaam kwa kutambua ujasiri wako na mifano yako hai ya uvumilivu, mafanikio na umahiri katika kupigania haki za wanawake na haki za watu wanaoishi na VVU na UKIMWI nchini.
Asanteni sana!
No comments:
Post a Comment