Mjumbe wa Baraza Kuu
la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko amefunga tawi la Chadema katika Kijiji
Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama
hicho cha siasa.
Tukio hilo limetokea jana tarehe
6th March 2014 katika kijiji cha Lukozi, wilaya ya Lushoto Mkoawa Tanga,
ambapo sambamba na kuasisi tawi hilo la Chama Cha Mapinduzi pia kiongozi huyo wa UVCCM
ameingiza wanachama wapya 206 ambapo wengi wao walikuwa ni wanachama wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mjumbe huyo wa Baraza Kuu
la Taifa la UVCCM, alifungua mashina sita yakiwemo ya Manyara, bodaboda, n.k pia alifanya vikao vinne vya ndani ambapo alizungumza na wana CCM juu ya hali ya Uimara wa
Chama na kuhoji kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Kijiji hicho ndani ya Wilaya ya Lushoto pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ambaoulihudhuriwanawananchiwengiwaLukozi.
Pamoja na vikao hivyo lakini pia Husna alitembelea vikundi vya ujasiriamali vya akina mama pamoja na kambi ya
JUDO ya Vijana wilayani Lushoto na kujadilinao Changamoto wanazokutananazo na kushirikiana nao kuzipatia ufumbuzi.
Husna anafanya ziara za kawaida katika Mkoa mzima wa Tanga katika kuhamasisha Vijana kujiunga na
Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya yaUmoja wa Vijana.
No comments:
Post a Comment